En cours de chargement...
Juma Ramadhan Magola Kilaza (Magola wa Chumbi), ambaye alijulikana zaidi kwa jina Kilaza ambalo ni jina la ukoo, ni mmoja kati ya wanamuziki bora kuwahi kutokea Tanzania. Mwanamuziki huyu, alianza kupiga muziki kwenye miaka ya 1960. Katika Maisha yake, alishiriki katika bendi za Morogoro jazz, Cuban Marimba, TK Lumpopo, Magola International na Les Cuban, zote za Morogoro akishiriki kupiga muziki unaojulikana zaidi kama muziki wa dansi ama rumba.
Kitabu hiki, kinasimulia maisha yake kimuziki, mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili, kuelimisha, kuburudisha, kuliwaza na kukuza sifa ya Morogoro. Kitabu pia, kinasimulia changamoto alizopitia, na visa vilivyovuma sana kati yake na mwanamuziki mwingine maarufu wa Morogoro Mbaraka Mwinshehe Mwaruka.